Kuelekea kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Bi. Karolina Mthapula ameendelea na ziara ya ukaguzi wa miradi itakayo zinduliwa na Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Simanjiro akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Simanjiro pamojana na Mkuu wa Wilaya hiyo Dk Suleiman Selela.
Katika ziara hiyo Katibu Tawala ametembelea Kata ya Kitwai katika kijiji cha Lodrekes ambako yatafanyika makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru ukitokea Wilaya ya Kiteto. Amefanya mazungumzo na wanakijiji cha Lodrekes akiwataka kujitokeza kwa wingi katika kuupokea Mwenge wa Uhuru utakapo wasili eneo hilo.
Aidha amefanya ukaguzi wa mradi wa barabara ya Jamhuri inayotarajiwa kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru Barabara iliyojengwa kwa kiwango cha rami, ambapo ujenzi wa barabara hiyo ni hatua ya kuboresha Halmashauri ya Simanjiro ujenzi huo umehusisha ujenzi wa karavati laini 9 ujenzi wa barabara hiyo umegarimu Milioni 572 ambapo barabara hiyo itaongeza mtandao wa barabara katika makao makuu ya Wilaya Simanjiro (Orkesumet) eneo ambalo ni makao makuu ya Wilaya hiyo.
Pia amefanya ukaguzi wa soko la Wilaya katika eneo lenye mradi wa uhifadhi taka sambamba na hilo amekagua eneo lenye mradi wa utunzaji wa mazingira ambako kunashughuli za upandaji miti eneo lenye hekali 5 ambapo matarajio makubwa katika mradi huo nikuwa eneo la mfano katika shughuli za utunzaji wa mazingira ambapo imepanda miti 127 katika eneo hilo.
Vilevile ametembelea nakufanyaukaguzi katika Hospitali ya Wilaya ya Simanjiro ujenzi wa mradi huo ulianza 28/3/2022 ujenzi huo nipamoja na jengo la wagonjwa mahututi (ICU) ujenzi huo utasaidia kusogeza huduma za Afya kwa wananchi wa Wilaya ya Simanjiro aidha Katibu Tawala Mkoa wa Manyara amefurahishwa na mradio huo kwa jinsi unavyoendelea.
Ametembelea nakufanya ukaguzi wa mradi wa josho ya kuoshea G’ombe iliyopo katika kijiji cha Ormoti ambapo josho hiyo itakuwa ikitumika kuoshea G’ombe zaidi ya elfu 21 mradi huo utasaidi kuepusha magonjwa ya mlipuko yanayo sumbua wafugaji katika kijiji cha Ormoti na kijiji cha Namalulu. Pia amefanya ukaguzi wa mradi mkubwa wa maji uliyokuwa ukitekelezwa na RUWASA katika Kata ya Emboreet amewashukuru RUWASA kwa mradi huo utakao ondoa tatizo la maji katika Kata hiyo na vijiji yake.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.