Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, vijana, ajira na watu wenye ulemavu Mhe. Profesa Joyce Lazaro Ndalichako. Amefanya ziara ya ukaguzi wa maandalizi ya shughuli za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru zinazo tarajiwa kufanyika tarehe 14 Oktoba mwaka 2023 Mkoa Manyara.Kabla ya ziara ya ukaguzi wa maandalizi Mh. Profa Joyce Ndalichako amefanya kikao na uongozi wa Mkoa wa Manyara kikao hicho kimefunguliwa na Katibu Tawala Mkoa wa manyara. Mhe. Karolina Mthapula katika ufunguzi wa kikao hicho ameipongeza Serikali kuleta shughuli za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Manyara.
Katika kuwasirisha taarifa fupi ya maandalizi mratibu wa mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Manyara Samwel Pastory ameeleza kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na yako kwenye hatua inayoridhisha. Akielezea kuhusu eneo muhimu la uwanja wa Kwaraa ambao ndio shughuli hiyo muhimu kitaifa itakapofanyika ameeleza juu ya ukamilishaji wa baadhi ya vitu kwenye uwanja huo ikiwa nimaendeleo mazuri yanayo onekana.
Pia Mhe. Joyce Ndalicahko amesema Uwanja wa Kwaraa umefikia hatua nzuri na mategemeo yake nikuona wananchi wa Mkoa wa Manyara wakijitokeza kwa wingi katika sherehe za kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru amepongeza ushirikiano uliyopo kati ya Serikali na Taasisi za Serikali zilizo Mkoa wa Manyara.
Katika ziara hiyo ametembelea uwanja ambao utafanyika uzinduzi wa maonesho ya wiki ya vijana kitaifa eneo la stendi ya zamani, Shule ya Sekondari Babati Day ambako mafunzo ya halaiki yanayoendelea. Pamoja na kanisa la Roho Mtakatifu ambalo litatumika katika ibada ya maadhimisho la Misa Takatifu kwa ajili ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.