Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. Suleiman Jaffo leo tarehe 03/09/2018 amefanya ziara ya kikazi Wilayani Hanang Mkoani Manyara na kufanya mkutano na watumishi wa wilaya hiyo. Akizungumza na watumishi Mh.Jaffo alisema utendaji wa kazi kwa sasa umebadilika tofauti na zamani hivyo watumishi hawapaswi kubweteka na wala kufanya kazi kwa mazoea pia aliwasisitiza wafanyakazi hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii ,wajenge mahusiano mazuri kati ya Idara na Idara ili kuhakikisha maendeleo yanapatikana.
Aidha aliwasisitiza wakurugenzi wa wilaya kuendelea kuwapima wafanyakazi hao kama wanafanya kazi vizuri na kama ikitokea wakashindwa kutimiza majukumu yao hawanabudi kuwaondoa na pia aliwataka watumishi hao kuacha ubinafsi, upendeleo na ufisadi wa rasilimali za wananchi na mapato ya serikali kwani Halmashauri yoyote haiwezi kuendeshwa bila mapato.
Vilevile Mh.Waziri alimtaka Mkuu wa Wilaya ya Hanang Mh. Joseph Mkirikiti kuunda timu ya kufanya uchunguzi juu ya ukusanyaji wa mapato na kuandaa taarifa sahihi juu ya mapato hayo, Mh. Jaffo alisema “hatuwezi kuruhusu fedha ziende kwa watu wachache kwani katika wilaya ya Hanang ukusanyaji wa mapato bado upo chini na miradi ya kimaendeleo bado hairidhishi hii ni kutokana na kukumbatiwa na watu wachache”.
Halikadhalika Mh. Jaffo alitoa onyo kwa viongozi waliochaguliwa, wabunge, madiwani na wenyeviti wa Halmashauri waache kuingilia maslahi ya Halmashauri kwa matumizi yao binafsi.
Akitoa neno la shukrani Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Alexander Mnyeti alisema “Utumishi ni maswala ya kujitolea hivyo watumishi ni jukumu letu kuwatumikia wananchi na kufanya kazi kwa bidii na maendeleo ya taifa pia alisema kikao hicho kimelenga kujenga, kuongoza na kuelimisha utendaji wa kazi za watumishi pia yale yote yaliyoelekezwa na Mheshimiwa Waziri tuyafanyie kazi na pia ni wajibu wetu kutumia sheria, kanuni na taratibu pia hekima na busara katika kuongoza wananchi.
(Kwa Picha mbalimbali na video angalia Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha na Maktaba ya Video)
Imeandikwa na Isabela Joseph (UDSM-Mafunzo kwa Vitendo)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.