Mikoa minane kati ya 26 nchini imepokea jumla shilingi za kitanzania bilioni 137,377,756,698. kwa ajili ya miradi utekelezaji wa miradi ya kimkakati nchini huku mgao huo ukienda sambamba na maelekezo mazito juu ya matumizi ya fedha hizo kutoka kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo.
Akitoa maelekezo hayo Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, Mhe. Selemani Jafo, alisema ni dhamira ya serikali ya awamu ya tano inayo ongozwa na Rais John Pombe Magufuli kuwaletea maendeleo wananchi wake, hivyo kwa Mikoa na Halmashuri zao ambazo zimepokea fedha hizo baada ya maandiko miradi yao kushinda suala kubwa na lakuzingatia ni juu ya matumizi sahihi na kuonesha thamani yafedha kwa kila mradi.
“Ajenda kuu ya Mhe. Rais, nikupambana na Rushwa na ubadhilifu wa aina zote hivyo kwa mikoa ambayo leo imeshinda katika maandiko ya miradi ya kimkakati na kupokea fedha hizi mhakikishe mnatumia fedha hizo kwa usimamizi wa hali ya juu na thamani ya fedha hiyo ionekane katika miradi manayokwenda kuitekeleza,” alisema Waziri Jafo.
Akisoma hotuba yake mbele ya Makatibu Tawala wa Mikoa hiyo, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri ambazo zimepata fedha hizo Jafo alisema, serikali katika awamu ya kwanza ya mwaka wa fedha wa 2017/18 na 2018/19 jumla ya Halmashauri 17 zenye miradi 22 zilifuzu vigezo na kuidhinishiwa jumla ya shilingi bilioni 131.46, huku akisikitishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo kwani kati ya fedha zilizokwisha tolewa ni bilioni 11.15 sawa na asilimia (33.23%) pekee ndizo ambazo zimekwisha tumika.
“Mwenendo unaonesha utumiaji wa fedha zilizo tolewa katika mwaka wa fedha wa 2017/18 ni Manispaa ya Morogoro pekee ndiyo iliyotumia kiasi chote cha fedha cha shilingi Bilioni 2.64 kwajili ya ujenzi wa soko ambalo lipo katika hatua za kufunga zege na kumwaga sakafu ya mwisho” wengine bado wana sua sua hii sio afya katika adhma njema ya serikali, Alisisitiza Waziri Jafo.
Aliongeza kuwa, sababu kubwa zinazo changia shughuli kwenda polepole ni pamoja na kutowashirikisha wadau, watendaji wengi kufanya kazi kwa mazoea, kukosa uthubutu wa kuandaa maandiko, kuchelewa kukamilisha michoro ya ujenzi pamoja na mivutano baina ya viongozi, ambapo amesema sababu hiyo ndio imekuwa mwiba mchungu katika kukamilisha miradi kwa wakati na kuonya juu ya kutoa kazi kwa kufahamiana baina ya wakandarasi na watendaji wa serikali na kusema kuwa katika awamu ya sasa atakaye thubutu kufanya hivyo hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake bila kumuonea aibu.
Mikoa iliyopokea mgao huo wa fedha za miradi ya kimkakati ni pamoja na Dar Es Salaam kwa Manispaa za Kinondoni iliyopata shilingi bilioni. 14,132,553,244 kwaajili ya uendelezaji wa fukwe, ujenzi wa soko katika Manispaa hiyo hiyo ya Kinondoni wamepewa kiasi cha shilingi bilioni. 9,697,126,000 Manispaa ya Kigamboni imepata mgao wa Bil.14,027,974,000 kwaajili ya soko la kisasa Kibada, wakati Mkoa wa Iringa kwa Manispaa ya Iringa shilingi 1,009,669,000 zimetolewa kwaajili ya ujenzi wa machinjia ya Kisasa.
Mikoa mingine ni Kagera katika Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo iliyopokea shilingi 2,817,960,672, kwaajili ya ujenzi wa kituo cha kuegesha magari makubwa, Mkoa wa Manyara kwa Halmashauri wa Wilaya ya Hanang iliyopokea shilingi 5,602,555,000 Halmashauri ya Wilaya ya Tarime wanaotekeleza mradi wa Soko la kisasa wamepokea shilingi 8,073,148,000 huku katika Mkoa wa Mwanza, Halmashauri ya Jiji la Mwanza, limepokea fedha kwa ajili ya miradi miwili ikiwa ni ujenzi wa soko la Mjini kati ambalo shilingi. 23,605,454,000 na shilingi shilingi 14,909,255,000 zimetolewa kwaajili ya Kituo cha Mabasi cha Nyegezi, wakati kwa Manispaa ya Ilemela mkoani hapo imepokea shilingi. 13,498,765 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha mabasi cha Nyamongolo na Shilingi 9,003,193,000 kwaajili ya ujenzi wa kituo cha kuegesha malori katika Manispaa ya Ilemela eneo hilo la Nyamongolo.
Aliongeza kuwa nikoa mingine ni Pwani na Tanga iliyo bahatika pia kupata fedha hizo za miradi ya kimkakati, ambapo, mkoani Tanga katika Halmashuri ya Jiji la Tanga, wamepata kiasi cha shilingi 8,854,779,839, kwaajili ya ujenzi wa kitega uchumi ndani ya kituo cha mabasi eneo la Kange. Wakati mkoani Pwani Halmashauri ya Bagamoyo imepata shilingi 1,600,000 kwaajili ya ujenzi wa Soko la Samaki- Chemchem, Halmashauri ya Kibaha katika kutekeleza ujenzi wa mradi wa Soko la kisasa Mlandizi imepokea shilingi 7,721,005,943 na Halmashauri wa Wilaya ya Kisarawe imepokea shilingi 2,824,318,000 ili iweze kutekeleza mradi wa kiwanda cha kubangua Korosho.
Kwa upande wao viongozi hao wa mikoa hawakusita, kuishukuru serikali kwa jitihada inazo endelea nazo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Said, alisema hatua ambayo serikali imechukua wanaipongeza na kudai kuwa fedha wanazo zipata ni zaidi hata makusanyo walio kuwa wanakusanya.
“Mhe. Waziri fedha ambazo sisi tumepokea kwakweli hata nusu tu ya makusanyo tunayofanya hayazifikii hivyo tunakila sababu yakuipongeza serikali, alisema Mhandisi Zena na kuongeza kuwa, mwanzoni walipokuwa wanaambiwa makusanyo yote yataenda hazina hawakulielewa somo hilo, lakini kutokana na matokeo ya sasa wameanza kuilewa serikali yetu inakusudia kufanya nini kwa watu wake.
Kwa upande Mstahiki Meya wa Kinondoni, Benjamin Sita, akishukuru kwa niaba ya Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri, alisema wanampongeza sana Mhe. Rais kwa jinsi anavyo itumikia nchi kwa moyo wa dhati na jukumu lililopo mbele yao nikuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana katika kusimamia kwa moyo wa kizalendo shughuli zote walizopewa dhamana kuzisimamia.
Mara baada ya hafla hiyo jopo hilo likiongozwa na Waziri wa Nchi OR TAMISEMI, lili zulu eneo inapojengwa Ofisi ya Wizara hiyo katika mji wa Serikali kwenye aneo la mtumba kwaajili yakujifunza namna yakutumia Force account eneo la mtumba.