Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe Charles Makongoro Nyerere akizungumza na walimu kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI) Mhe.Angellah J. Kairuki katika kikao kazi cha uboreshaji wa usimamizi wa Elimu Msingi na Sekondari, kilichowakutanisha maafisa Elimu Wilaya na Kata, wakuu wa shule za sekondari, na walimu wakuu wa shule za msingi Mkoa wa Manyara.
Alisema wapo baadhi ya watumishi wanaotoa lugha chafu ambazo zinarekodiwa na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, na kwamba Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan haiwezi kumvumilia mtumishi wa aina hiyo.
RC Makongoro amewataka wahakikishe wanafunzi wanapata umahiri wa stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu wamalizapo darasa la kwanza, na kwamba ufundishaji wa somo la kiingereza unaimarishwa kwa shule za msingi na Sekondari.
Aidha,Amewataka viongozi wa Elimu ngazi ya shule, kata, halmashauri na mikoa kuhakikisha wanafuatilia ufundishaji wa walimu darasani pamoja na kutatua kero za walimu kwenye maeneo yao ya kazi badala ya kukaa maofisini.
Naye Naibu Katibu Mkuu(ELIMU) Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Charles E. Msonde amesema ili watoto wabaki salama lazima kila mmoja awe mlinzi wa mtoto na kuona kuwa ni mtoto wake
Akitoa salamu za Mkoa wa Manyara Katibu Tawala Mkoa wa Manyara Bi.Karoline Mthapula alisema kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Mkoa wa Manyara ulipokea kiasi cha Tsh. 3,760,000,000.00 kwaajili ya ujenzi wa shule mpya 8 za Kata kupitia mradi wa (SEQUIP). Shule 7 kati ya shule 8 zimesajiliwa na zimepokea wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2023.
Aidha, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023 Mkoa wa Manyara ulipokea kiasi cha Tshs. 1,540,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 77 vya shule za Sekondari. Hadi sasa Mkoa umekamilisha ujenzi wa vyumba vyote 77 vya madarasa sawa na asilimia 100.
Mthapula alisema hadi kufikia tarehe 10 Januari, 2023, Mkoa umeandikisha wanafunzi wa Elimu ya Awali 29,864 ambapo wavulana ni 15,564 wasichana 14,300100
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.