Mkuu wa Mkoa wa Manyara amewataka Maafisa Ardhi wake kuhakikisha wanamaliza migogoro ya Ardhi kwa wananchi ili kuwafanya wananchi wa Mkoa wa Manyara kuishi bila migogoro katika Mkoa huo.
Hayo aliyasema Leo wakati wa kikao cha Maafisa Ardhi wa Halmashauri zote saba zilizopo katika Mkoa huo.
Katika kikao hicho Mh.Mnyeti alisema kuwa Mkoa wa Manyara ni miongoni mwa Mikoa inayoongoza kwa migogoro ya Ardhi nchini Tanzania kwa hivyo ni lazima Maafisa Ardhi wahakikishe wanamaliza migogoro hiyo angalau kwa asilimia themanini.
“Sasa hivi tukigundua Afisa Ardhi amesababisha migogoro isiyokuwa na maana hatutamuhamisha bali atashughulikiwa katika Halmashauri hiyo aliyovurunda” Mh. Mnyeti alisisitiza.
Pia katika kikao hicho aliwakikishia wananchi wa Maisaka Katani kuwa ifikapo Octoba 26 watapatiwa Hati Miliki za maeneo yao kama alivyoiagiza Halmashauri ya Mji wa Babati alipofanya ziara katika ziara yake katika Halmashauri hiyo.
(Baadhi ya wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mh.Alexander Mnyeti wakifuatilia kikao cha Mkuu Mkoa wa Manyara akiongea na Maafisa Ardhi wa Mkoa wa Manyara 30 Augusti,2018.)
(Mkuu wa Mkoa wa Manyara (wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Ardhi wa Mkoa wa Manyara 30 Augusti,2018.)
(Kwa Picha mbalimbli na Video za matukio angalia Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha na Maktaba ya Video)
Imeandikwa Na: Haji Athumani (Afisa Habari Mkoa wa Manyara)
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.