Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Cuthbert Sendiga Akiwa kwenye ziara katika Kijiji cha Endadoshi Kata ya Qash wilayani Babati alipokea kero ya ukosefu wa zahanati Kijijini hapo hali inayowafanya wananchi wa eneo hilo watembee umbali wa Km 20 kufata huduma za matibabu katika zahanati ya Kijiji Jirani.
Katika kutatua changamoto hiyo RC Sendiga aliahidi kutoa saruji mifuko 100 kwa ajili ya kuanzisha ujenzi wa Zahanati. Katika kuunga mkono hamasa ya Mkuu wa mkoa, naye Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa jimbo hilo la Babati Vijijini Mhe. Daniel Sillo aliahidi kuchangia saruji mifuko 50
Aidha, wananchi nao walihamasika na miongoni mwa waliokuwapo kwenye mkutano huo wa hadhara walijitokeza kumuunga mkono Mkuu wa mkoa na kufanikisha kupatikana vifaa vya ujenzi kwa ujumla wa Saruji mifuko 610, Bati 170 na Tripu 10 za mawe.
Mhe RC aliwashukuru na kuwapongeza kwa moyo wao wa kizalendo wote waliojitokeza kuchangia vifaa hivyo vya ujenzi na ameahidi kuifuatilia na kusimamia ujenzi wa zahanati hiyo hatua kwa hatua.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.