Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa Mzee Mkongea Alli amewataka wazazi kuacha tabia ya kuwaozesha watoto wa kike mapema, kwani kitendo hiko kinawanyima fursa nyingi za maendeleo.
Akizungumza mara baada ya kuzindua mradi wa madarasa 8 na ofisi 3 katika Shule ya msingi Bacho kata ya Dareda halmashauri ya wilaya ya Babari, alisema kitendo chabkumuozesha mtoto wa kike mapema ni kumnyika haki yake ya msingi.
Alisema wazazi wana jukumu la kuhakikisha anamsimamia kikamilifu mtoto wake wa kike ili kuweza kumsaidia kutimiza wajibu wake ili kutimiza nankufikisha ndoto za mtoto katika kuhakikisha anatimiza malengo yake ya kusoma kikamilifu, na si vingine.
" Wazazi wenzangu tuache tabia ya kuwaozesha mapema watoto wetu, hili ni tatizo kubwa sana ambalo litawanyima fursa watoto wa kike kutokusoma, unapomuozesha mtoto wa kike mapema bila ridhaa yake unamvunjia fursa nyingi sana za maendeleo , unamsababaishia maambukizi ya VVU Ukimwi, unamsukumiza kwa mtu ambaye hana interest naye, hamuelewi, lakini pia kunapelekea vifo vya mama na mtoto" alisema Mkongea Ali
Aidha aliwataka walimu kutunza miundombinu hiyo kwani wahisani walijitokeza kujenga miundombinu hiyo kwakua waliona utendaji wao wa mzuri wa kazi, hivyo wametakiwa kuhakikisha wanatunza miundombinu hiyo ili wahisani wapate moyo wa kutoa zaidi ya walichotoa kwani wametumia pesa nyingi kukamilisha Ujenzi wa Mardi.
Aidha aliwapongeza wahisani waliojenga mradi huo pamoja na wananchi kwa kuchangia nguvu kazi zao kwa kuhakikisha wanawawekea miundombinu mizuri ya elimu ili watoto waweze kusoma katika miundombinu mizuri.
" Niwashukuru wananchi kwa nguvu zenu ni kazi Nzuri sana ambayo tumeiona, lakini pia niwashukuru wafadhili wetu ambao wamefadhili kwa kiasi kikubwa sana kuhakikisha wanatuletea miundombinu mizuri ya elimu ili watoto wetu wapate wlimu bora, hivyo wananchi nadhani mmejionea miundombinu mizuri sana inavutia yaani unapoingia darasani unatamani mwalimu awepo afundiishe" alisema
Aidha aliwageukia wanafunzi kuhakikisha wanajijengea mazingira ya kupenda kusoma ili kuweza kutimiza ndoto zao, kwani hatma ya maisha yako iko mikononi mwao, hivyo wana kila sababu ya kuhakikisha kuwa wanasoma kwa bidii ili kuwatia moyo wazazi wanaowasomesha.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Babati mkoani Manyara Elizabert Kitundu wakati wa makabidhiano ya mwenge wa uhuru kutoka kwa mkuu wa wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga alisema jumla ya miradi 7 yenye thamani ya zaidi ya mil.600,ambayo imetembelewa, kuzinduliwa, kuwekewa jiwe la msingi katika halmashauri hiyo.
Aidha Kitundu alifafanua kuwa Mwenge wa Uhuru ulikimbiza kwa umbali wa km. 150, huku wananchi wakichangia sh .mil. 96.8 , halmashauri wamechangia sh.mil. 8.6, serikali kuu imechangia sh.mil. 370.9 huku wahisani wakiwa wamechangia sh.mil.167.1
Hata hivyo Kiongozi huyo alimtaka mkuu wa wilaya huyo kuhakikisha anaendelea kuifuatilia miradi mbalimbali inayoendelwa katika wilaya yake.
Katika hatua nyingine Kiongozi huyo aliupongeza uongozi wa Shule ya sekondari kwa kuwafundisha wanafunzi nyimbo nzuri ya uchaguzi wa serikali za mitaa, kufuatia wimbo huo amemtaka mkuu wa wilaya hiyo Elizabert Kitundu kuhakikisha anaufuatilia wimbo na kuhakikisha unarekodiwa ili ifikapo siku ya uchaguzi wimbo huo uweze kutumika.
(Kwa picha mbalimbali angalia sehemu ya Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha)
Imeandikwa na:Haji A.Msovu
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.