• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Huduma za Maji
    • Kitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Procurement
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Huduma ya Maji
    • Kilimo
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Strategic Plan
    • Huduma ya Makubaliano ya Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Habari
  • Blog

ALEXANDER MNYETI AKUTANA NA WADAU WA MAENDELEO MANYARA

Imechapishwa Tarehe: June 20th, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh.Alexander Mnyeti leo amekutana na wadau mbalimbali wa maendeleo Mkoani Manyara katika kikao kilichoitishwa katika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la Mkuu wa Mkoa ili kujadili fursa mbalimbali zipatikanazo katika Mkoa huo.

Akiongea katika kikao hicho kilichohudhuriwa na wadau wa maendeleo kutoka wilaya zote tano za Mkoa huo Mh.Mnyeti aliwahimiza wadau hao kujitokeza kuanzisha viwanda vipya na kufufua viwanda vilivyokufa hasa katika maeneo ya kilimo,ufugaji,misitu,madini na utalii Mkoani Manyara kwani malioghafi za viwanda zinapatikana kwa urahisi Manyara na pia kutaewaletea ajira wananchi wa Manyara na Tanzania kwa ujumla.

Mh. Mkuu wa Mkoa pia alisisitiza kuwa ifikapo Disemba Mwaka 2018 Mkoa wa Manyara itafikia lengo la kuanzisha viwanda 100 ili kutimiza ahadi ya Rais kuwa kila Mkoa kuwa na viwanda 100 kwani mpaka sasa mkoa umeanzisha viwanda 68 kati ya 100 vinavyohitajika.

Vilevile Mh.Mnyeti alizitaka Halmashauri zote saba zilizopo Mkoanio kwake kuhakikisha zinatenga asilimia tano kwa ajili ya vijana na kinaMama na kuwakopesha bila riba ili kuwawezesha kujikwamua na umaskini.

Akiwasilisha mada katika kikao hicho Mtaalam kutoka TIRDO Dkt.Mushi aliwaambia wadau wa maendeleo kuwa Mkoa wa Manyara ni miongoni mwa mikioa yenye hali ya hewa nzuri inayokubali kila aina za mazao hivyo kuwahimiza kuwekeza mkoani humo.

Wakichangia mada wadau wa maendeleo mkoani humo wamemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwaita na kuwaleta wataalam kutoka TIRDO ili kuwafahamisha fursa mbalimbali zipatikanazo mkoani humo.

Mkoa wa Manyara una fursa kama za kilimo cha Mahindi,ufuta,alizeti,mtama,ngano na maharage pia wawekezaji wanaweza kuwekeza kwenye viwanda vya kusindika bidhaa hizo.vilevile kuna fursa za kuanzisha machimbo ya madini, viwanda vya chumvi,viwanda vya Saruji, viwanda vya asali pamoja na viwanda vya mazao ya misitu.

Imeandikwa na: Haji A.Msovu(Afisa Habari Mkoa wa  Manyara)

Matangazo

  • RATIBA YA MITIHANI KIDATO CHA SITA 2019 February 08, 2019
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2019 MANYARA December 17, 2018
  • Matokeo upimaji Kidato cha Pili 2018. January 05, 2019
  • MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2018 MKOA WA MANYARA December 27, 2017
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • Jafo Akabidhi Bilioni 137 kwa Mikoa 8

    February 07, 2019
  • Jafo aonyesha mfano wa matumizi bora ya Force Account

    February 07, 2019
  • Jafo alaani watumishi kutumia nguvu dhidi ya wananchi

    February 06, 2019
  • Misri kuwekeza kwenye kilimo nchini

    February 06, 2019
  • Tazama Zote

Video

Manyara ya pili Kitaifa Miradi ya Maendeleo
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

    Singida Road

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 310

    Simu ya mezani: 027-2510066

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: rasmanyara@manyara.go.tz

Mawasiliano mengine

   

Idadi ya Waliotembelea

https://Dissertation-Writingservice.com

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Sitemap

Haki zote zimehifadhiwa @2017 Mkoa wa Manyara