• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • Malalamiko |
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Kilimo
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Fomu za Kujiunga na Bangdalalu Sekondari
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Habari
  • Blog

Vijana Kiteto wanufaika na Mikopo ya Halmashauri

Imechapishwa Tarehe: January 5th, 2021

Vijana Wilayani  Kiteto wameishukuru Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Kiteto kwa kuwawezesha kupata mikopo isiyokuwa na riba ili na kuweza  kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

Hayo yamesemwa na vikundi mbalimbali vya Vijana, wanawake na walemavu Wilayani Kiteto mara walipotembelewa na Maafisa kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI walipokuwa wakitembelea na kukagua matumizi ya asilimia kumi na jinsi zinavyogawanywa kwa makundi husika.

Akiongea wakati walipotembelewa na Maafisa hao kutoka TAMISEMI Mwenyekiti wa  Kikundi cha Kiteto Vijana Agro Business kinachojihusisha na ulimaji wa mboga na ufugaji wa samaki Bwana Charles Joseph amesema walijiunga vijana hamisini na kuanza kulima bustani na baadae walipewa  msaada wa kujengewa Kitalu Nyumba  chenye thamani ya Shilingi Milioni Kumi na sita na Ofisi ya waziri Mkuu na baadae kupewa mkopo wa milioni kumi na sita na Halmashauri kupitia asilimia nne za vijana na kujenga kitalu nyumba kinginge kwenye eneo walilopewa na Halmsahuri ya Kiteto na kuanza kulima nyanya.

"Kwa hatua hii tuliyofikia sisi kama vijana tumejipanga kuhakikisha tunafanikiwa kupitia mikopo hii kutoka Halmashauri na tutajitahidi kufanya marejesho kila mwezi ili kuongeza uaminifu kwa viongozi wetu" Alisema Bwa Charles.

Pamoja na vijana hao kuishukuru Serikali kwa mikopo hiyo pia wameelezea changamoto mbalimbali wanazokutana nazo ikiwemo magonjwa na upatikana wa soko.

Akijibu haja ya changamoto  magonjwa Mchumi kutoka TAMISEMI Bwana.Fulgence Matemele aliwata maafisa kilimo kuwatembelea vijana hao mara kwa mara ili kuhakikisha wanapata viwatilifu vya kujinga na mbogamboga hizo ikiwemo kuwatafutia soko la bidhaa zao hata nje ya Kiteto.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu Wilaya ya Kiteto Bwana Marsi Kisarika Urassa ambaye anafuga kuku amesema kuwa yeye kama mlemavu anaishukuru sana Halmashauri ya Kiteto kwa mkopo aliyopewa na kuwashauri walemavu wenzake wasibweteke kwa kuwa ni walemavu kwani ulemavu sio sababu ya kutokufanya kazi.

Bwana Urassa ambaye ni mlemavu wa Mguu na mkono  kupitia mkopo huo ameweza kufuga kuku zaidi mia moja na kulimiki shamba la ekari kumi.

Akielezea changamoto za walemavu kupata mkopo Halmashauri Bwana Urassa alisema kuwa tatizo kubwa ni kuwa walemavu wanatakiwa kujiunga katika vikundi ili kuanzisha miradi lakini tatizo kubwa ni ulemavu unatofautiana.

"Tunashindwa kujiunga katika vikundi kwa kuwa unaweza kuta kila mtu ana ulemavu tofauti kwa hiyo tunashindwa kuanzisha mradi mmoja, tungeomba serikali iangalie sheria upya ili sisi walemavu tuweze kupewa Mikopo kwa mmoja mmoja" Alisisitiza Bwana Urassa.

Akitoa ufafanuzi kuhusu sheria za walemavu kupewa  mikopoa binafsi Afisa rasilimali fedha kutoka TAMISEMI  bwana.Ismail Chami amesema kuwa sheria itabadilishwa ili  walemavu waweze kukopa mikopo binafsi ili kila mlemavu aanzishe mradi wake kulingana na ulemavu unaomkabili.

Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imeamua kupitia kila Halmashauri nchi nzima kuona jinsi mikopo ya asilimia nne kwa wanawake, asilimia nne kwa vijana na asilimia mbili kwa walemavu inavyotolewa na kuhakikisha mikopo hiyo inatolewa bila ya riba.

Matangazo

  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA 2021 MKOA WA MANYARA December 18, 2020
  • MAJINA YA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO LA BABATI MJINI October 21, 2020
  • MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2018 MKOA WA MANYARA December 27, 2017
  • OR-TAMISEMI YATANGAZA AJIRA MPYA ZA WALIMU WA MSINGI NA SEKONDARI JULAI 2018 July 17, 2018
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • Vijana Kiteto wanufaika na Mikopo ya Halmashauri

    January 05, 2021
  • Babati watakiwa kuchangamkia Mikopo ya Serikali

    January 04, 2021
  • Waziri wa Kilimo awataka Wakulima wa ngano kuongeza uzalishaji

    December 24, 2020
  • Njooni muwekeze Manyara- RC Manyara

    December 22, 2020
  • Tazama Zote

Video

Nangwa Sekondari katika muonekano mpya
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

    Barabara ya Babati - Singida

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 310

    Simu ya mezani: 027-2510066

    Simu ya kiganjani:

    Barua pepe: rasmanyara.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2020 Manyara Region . All rights reserved.