Mkoa wa Manyara una eneo la hekta 1,568,117 zinazofaa kwa kilimo ambapo zaidi ya hekta 867,500 zinatumika kwa kilimo cha mazao ya aina mbalimbali. Eneo la kilimo linabadilika kila msimu kulingana na malengo ya wakulima na mwelekeo wa hali ya hewa.
Pia Mkoa una maeneo yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji yanayofikia hekta 30,997 na kati ya hizo hekta 11,715 zinatumika kuzalisha mazao ya aina mbalimbali kama vile mahindi, mpunga, miwa, migomba na mazao ya mbogamboga na matunda. Maeneo makubwa yapo Wilaya ya Babati (Bonde la Kiru) na Simanjiro (Ukanda wa Mto Pangani). Maeneo mengine yapo Mbulu (Bonde la Bashay) na Hanang (Bonde la Endagaw na Gocho)
Mazao yanayolimwa ni Mahindi, Alizeti, Mbaazi, Mtama, Ngano, Maharage, Miwa, Vitunguu Maji, Vitunguu Saumu na Mpunga ambayo hutumika kama mazao ya Biashara na Chakula kwa wakazi wa Mkoa. Ziada ya uzalishaji huuzwa kwenye Mikoa mingine na Nchi jirani za Kenya, Somalia, Ethiopia, Eritrea na Sudani.
Moja ya Mashamba ya Mahindi Wilayani Hanang-Mkoa wa Manyara
Moja ya Mashamba ya Mbaazi Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara
Moja ya Mashamba ya alizeti katika Wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara
Shamba la Ngano katika Wilaya ya Hanang-Mkoa wa Manyara
Mafanikio yaliyopatikana katika Sekta hii yanatokana na jitihada za Serikali na wadau wa maendeleo katika kuimarisha matumizi ya wanyama kazi, matrekta makubwa na madogo (power Tillers), mbegu bora, mbolea na wataalam wa ugani.
Maksai wakitumika kusafirisha mazao shambani
Mwaka 2006, Serikali ilianzisha Mpango wa kilimo wa ASDP kwa lengo la kuongeza uzalishaji mazao kwa kushirikiana na Mradi wa PADEP “Participatory Agriculture Development and Empowerment Project” unaoshirikisha wananchi kuibua Miradi ya Vikundi na Miradi ya Jamii na kuchangia gharama za utekelezaji katika Sekta za Kilimo na Mifugo.
Miundombinu mbalimbali iliweza kujengwa katika maeneo mengi ya Mkoa.
Baadhi ya miundombinu hiyo ni Vituo vya rasilimali za Kilimo na Mifugo, Maghala, majosho, nyumba za maafisa ugani na machinjio.
Aidha, Mkoa unashirikiana na Mashirika na Taasisi za Maendeleo ya kilimo katika kukuza na kuendeleza Sekta ya Kilimo na Mifungo. Mashirika hayo yametajwa katika jedwali lifuatalo na kuonesha majukumu wanayotekeleza.
Mashirika na Taasisi za Maendeleo katika Kilimo
NA
|
SHIRIKA
|
MAJUKUMU
|
ENEO LA UTEKELEZAJI
|
1.
|
Farm Africa
|
Kuimarisha uzalishaji wa Kilimo na Mifugo
|
Babati, Hanang’ na Mbulu
|
2.
|
World Vision
|
Kuendeleza Sekta za Mifugo, Kilimo.
|
Simanjiro na Babati
|
3.
|
FIDE
|
Kutoa Mafunzo katika Sekta za Kilimo, hifadhi ya Mazao, Ufugaji, Teknolojia ya biogas.
|
Babati
|
4.
|
TRIAS
|
Hutoa ufadhili wa fedha kwa Mashirika mengine 13
|
Babati na Mbulu
|
5.
|
FAIDA Mali
|
Hutoa mafunzona kuwaunganisha wazalishaji na Masoko
|
Babati na Hanang
|
6.
|
SARI
|
Utafiti katika uzalishaji wa Kilimo na Mifugo.
|
Wilaya zote za Mkoa
|
7.
|
SNV
|
Kujenga uwezo, Kutoa Ushauri, kuu nganisha wadau mbalimbali wa Maendeleo
|
Wilaya zote za Mkoa
|
8.
|
MVIWATA
|
Uundaji vikundi vya wakulima, elimu ya Kilimo na Masoko
|
Wilaya zote
|
9.
|
MAI
|
Kuimarisha Kilimo na Mifugo
|
Wilaya zote za Mkoa
|
10
|
African Rising
|
Kuimarisha Malisho Bora
|
Babati
|
11
|
COSITA
|
Kuimarisha Kilimo cha Ufuta
|
Babati
|
12
|
AFAP
|
Kuboresha kilimo cha maharage na Soya
|
Babati na Hanang
|
13
|
TAHA
|
Uboreshaji wa Kilimo cha Mbogamboga na Matunda
|
Babati, Hanang na Mbulu
|
14
|
PRISE
|
Utafiti wa athari za mabadiliko ya tabianchi
|
Simanjiro
|
15
|
Maisha Bora
|
Maboresho katika huduma za Mifugo, Maji na Ujasiriamali
|
Simanjiro
|
16
|
MEDA
|
Uwekaji wa Vitamin A kwenye mafuta
|
Babati
|
17
|
SIDO
|
Uwezeshaji wa wajasiriamali katika usindikaji mbalimbali na ubunifu
|
Wilaya zote
|
18
|
TPRI
|
Utafiti na Ushauri katika masuala ya viuatilifu
|
Wilaya zote
|
SEKTA YA MIFUGO
Baadhi ya wanyama wafugwao Mkoani Manyara
Mkoa una zaidi ya mifugo milioni 3. Kati ya hao ng’ombe wa asili ni 1,747,683; ng’ombe wa kisasa ni 22,485; Mbuzi wa asili ni 1,411,752; mbuzi wa kisasa ni 27,346; Kondoo wa asili ni 576,889 na wa kisasa ni 10,317; Nguruwe ni 79,696; kuku wa asili ni 1,176,901 na wa kisasa ni 20,813 na punda ni 64,385. Hakika huu ni utajiri mkubwa. Sekta hii pekee imeajiri zaidi ya asilimia 11 ya wakazi wa Mkoa.
Yapo maboresho mbalimbali yaliyofanywa na Serikali kwenye sekta kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo. Maeneo yaliyofanyiwa kazi ni uboreshaji wa kosaafu kwenye kupitia madume bora, ujenzi na ukarabati wa majosho.
Mafanikio ya Sekta ya Mifugo yameongeza uzalishaji wa nyama kutoka kilo 150 hadi kilo 300 kwa ng’ombe mzima na maziwa kutoka wastani wa lita 1 hadi lita 5-10 kwa siku.
Josho lililoko Wilayani Babati Mkoa wa Manyara
Kutokana na Mafanikio hayo, Mkoa una fursa nyingi za kuwekeza katika sekta ya ufugaji hususani uanzishaji wa ranchi na viwanda vidogo vya kusindika mazao ya mifugo kama ngozi, maziwa na nyama. Fursa nyingine ni ujenzi wa majosho na mabwawa. Halmashauri za Mkoa zimetenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji wa aina mbalimbali.
UVUVI
Uvuvi katika Mkoa wa Manyara ni moja ya sekta inayo changia katika kukuza uchumi na kupunguza umasikini kama ilivyo ainishwa katika MKUKUTA.
Mchango wa shughuli za uvuvi katika Mkoa wa Manyara ni mkubwa kwani imetoa ajira kwa watu takribani zaidi ya 1800 wakiwemo wavuvi, wachuuzi wa samaki na wafugaji wa samaki,
Samaki ni chanzo cha protini itokanayo na wanyama, chanzo hiki cha protini ni Muhimu kwani walaji wenye kipato cha chini ambao hawawezi kumudu vyanzo vingine vya protini wanaweza kumudu chanzo hichi kikilinganishwa na vyanzo vingine vya protini itokanayo na wanyama,
Rasilimali za uvuvi katika Mkoa wa Manyara zinapatikana katika maeneo ya wilaya za Babati, Hanang, Mbulu na Simanjiro katika maeneo ya bwawa la nyumba ya mungu, ziwa Babati, ziwa Burunge, Ziwa Manyara na ziwa Bassotu.
Ukuzaji wa viumbe katika maji kwa maana ya ufugaji wa samaki katika mabwawa ya kuchimbwa na yale ya asili ( malambo) pia unafanyika katika Halmashauri zote za mkoa wa Manyara ambapo kuna jumla ya Mabwawa ya samaki yapatayo 121 na malambo 8 yenye samaki.
Baadhi ya zana za uvuvi katika Bwawa la Nyumba ya Mungu
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.