• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

Maafisa ugani Manyara wapata mafunzo ya kukabiliana na Nzige

Imechapishwa Tarehe: February 18th, 2020

Wataalam wa Wizara ya Kilimo  wametoa mafunzo ya kukabiliana na namna ya kuwatambua Nzige wa Jangwani ambao wamekuwa wakishambulia mimea katika nchi za Kenya, Uganda na Ukanda wa Kaskazini mashariki mwa bara la Afrika na janga la Nzige  kwa Maafisa Kilimo na Maafisa Maendeleo ya Jamii Mkoani Manyara.

 Bw. Juma Mwinyimkuu kutoka Kitengo cha Afya ya Mimea Kanda ya Kaskazini aliwaeleza washiriki kuwa Nzige ni wadudu hatari endapo watatua kwa makundi makubwa kwenye eneo moja kwa kuwa kila nzige moja ana uwezo wa kula mimea kiwango cha uzito wake kwa siku na ambayo ni sawa na gramu 20, hivyo kundi la Nzige laki tano wana uwezo wa kula Tani moja kwa siku. Alieleza kuwa Nzige hutembea katika makundi yenye wastani wa nzige milioni 10 hadi milioni 50 au Zaidi hivyo wanapotua katika eneo lenye mimea, mazao au misitu husabisha uharibifu mkubwa.

“Kila Nzige jike ana uwezo wa kutagaa mayai Zaidi ya 200 ndani ya kipindi cha wiki moja panapokuwa na mazingira ya unyevu,hivyo tahadhari inayotolewa ni kuwabini nzige hata wakiwa wachache ili kudhibiti uzalianaji wao kabla hawajawa kundi kubwa” Alisema Mtaalam huyo.

Kwa upande wa Mtaalam wa TPRI kitengo cha Unyunyiziaji wa Viuatilifu Bw. Justin Ringo aliwaeleza washiriki kuwa sumu inayotumika kuwadhibiti ni aina Fentrothion 96% ambayo iko chini ya Kundi la viuatilifu aina ya Organophosphate. Alisema kiuatilifu hicho kinasimamiwa na Wizara ya Kilimo na haiuzwi kwenye maduka ya Pembejeo. Aliwashauri wataalam hao kuhakikisha wanatoa elimu juu ya matumizi ya kiuatilifu hicho (Fentrothion 96%) na kuwaelimisha watumiaji kuchukua tahadhari kwa kuvaa mavazi maalum (overali+cloves, miwani maalum ya kulinda macho na viatu ili wakati wa kupulizia wadudu kwenye shamba mtu asiguswe na sumu kwenye ngozi ya mwili kwa kuwa sumu ikiingia kwenye mishipa ya damu inaleta madhara.

Alielezea upigaji wa sumu hiyo kwa njia mbili; njia ya kwanza ni kutumia aina tofauti ya mabomba maalum yanayobebwa mgongoni lakini aina ya pili ni kwa mashamba makubwa ambapo ndege maalum inatumika kupuliza kiuatilifu kutoka angani,lakini lazima kusiwe na watu au wanyama ambao wanaweza kudhuriwa na kiuatilifu hicho.

Wito ulitolewa kwa wataalam walioshiriki mafunzo hayo kwenda kusambaza ujumbe huo wa kuwatambua nzige wa jangwani na kutoa taarifa kutoka kwenye Vijiji, Kata kwenda Halmashauri, Mkoa na hatimaye Wizara ya Kilimo kwa ajili ya kuchukua hatua za haraka za kusambaza viuatilifu na vifaa vya kupigia viuatilifu.

Mafunzo hayo yametolewa baada ya kutokea sintofahamu ya uvamizi wa Nzige nchini Tanzania hasa Mkoa wa Kilimanjaro.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.