Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe.Joseph Mkirikiti amewapongeza wafanyakazi wote wa Wakala wa Maji Vijijini RUWASA Mkoa Manyara kwa kujitahidi kufikisha huduma ya maji Mkoani humo.
Mhe.Mkirikiti ametoa pongezi hizo leo alipokuwa akipokea taarifa ya ukaguzi wa miradi ya maji Mkoani humo katika kikao Kati yake na wafanyakazi wote wa Mamlaka hiyo Mkoani humo kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Akisoma taarifa ya miradi ya maji Mkoani humo Meneja wa RUWASA MKoa wa Manyara Mhandisi Wolta Kirita amesema kuwa mkoa wa Manyara umetengewa Shilingi Bilioni 13.4 kwa ajili ya kukamilisha miradi 45 kwenye Wilaya zote za Mkoa na miradi na mara baada ya miradi hiyo kukamilika na vituo 632 vitakarabatiwa na kujengwa na kuwanufaisha watu zaidi ya 156,903 na mara baada ya kukamilika itapunguza Vijiji visivyo na maji kutoka 163 hadi 118.
Pamoja na kutoa taarifa ya miradi hiyo na kuonesha jinsi RUWASA inavyofanya ili kuhakikisha wanatimiza ahadi ya Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli ya kumtua Mama ndoo kichwani Meneja wa RUWASA Mkoa alisema wanakumbana na tatizo la umeme.
"Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa pamoja kuhakikisha tu maji yanafika katika maeneo mengi ya mkoa wetu lakini kuna changamoto ya umeme katika baadhi ya vituo"Alisema Mhandisi Kirita.
Mara baada ya kopokea taarifa hiyo Mkuu wa Mkoa Mhe.Joseph Mkirikiti amewapongeza RUWASA kwa kufanya kazi kwa bidii na sehemu kubwa ya Mkoa wa Manyara unapata huduma ya maji.
"Kiukweli RUWASA katika Mkoa wetu mnafanya kazi nzuri mno na mnahitaji pongezi"Alisema Mhe.Mkirikiti.
Pamoja na kutoa pongezi hizo alizitaka taasisi nyingine zote zilizopo Mkoani Manyara kuhakikisha zinaiga kutoka kwa RUWASA katika kuwapa Wananchi huduma nzuri.
Baada ya kusomewa taarifa ya miradi katika Mkoa Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa alitembelea katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang kwa kutembelea Dawar,Hilbadaw, Waranga na Endagaw kuangalia jinsi miradi ya maji inavyotekelezwa na kuwafikia Wananchi ili kuondoa tatizo la maji Mkoani Manyara.
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa kesho ataendelea kukagua miradi ya maji Mkoani humo kwa kutembelea Wilaya ya Mbulu.
Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.