• Maswali ya Mara kwa Mara (MMM) |
    • Barua pepe za Wafanyakazi |
    • e-Mrejesho |
Manyara Regional Secretariat
Manyara Regional Secretariat

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Sekretarieti ya Mkoa wa Manyara

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Sehemu
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za Elimu
      • Serikali za mitaa
      • Huduma za Afya
      • Utawala na Rasilimali Watu
    • Vitengo
      • Uhasibu
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi
      • TEHAMA
  • Wilaya
    • Babati
    • Mbulu
    • Hanang
    • Kiteto
    • Simanjiro
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Mji wa Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Babati
    • Halmashauri ya Wilaya ya Hanang'
    • Halmashuri ya Wilaya ya Mbulu
    • Halmashauri ya Mji Mbulu
    • Halmashauri ya wilaya ya Kiteto
    • Halmasahuri ya Wilaya ya Simanjiro
  • Fursa za uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
    • Madini
    • Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Maji
    • Huduma za Elimu
    • Huduma kwa wateja
    • Huduma kwa wafanyakazi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sheria Ndogondogo
    • Ripoti
    • Mpango Kazi
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Picha
    • Hotuba
    • Video
    • Habari

TANAPA YAZINDUA MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI KWA MIKOA MITATU

Imechapishwa Tarehe: August 15th, 2018

Hifadhi ya Taifa ya Tanzania  (TANAPA) kwa kushirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii umezindua  Utekelezaji wa mpango wa Matumizi  ya Ardhi   ya Vijiji vinavyopakana na hifadhi za Taifa ili kupunguza migogoro ya matumizi ya Ardhi.

Mpango huo ambao unalengo la kutatua migogoro ya Ardhi kati ya wananchi na Hifadhi  utakaoshirikisha Mikoa mitano ya Manyara, Dodoma, Mara, Arusha na Simiyu  iliyozungukwa na hifadhi za Taifa umewakutanisha Viongozi wa  Mikoa hiyo leo Mkoani Manyara ili kuzindua na kujadili utekelezaji wa Mpango huo.

Aidha Mkutano huo ulihudhuriwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Willium Lukuvi na Naibu waziri Maliasili na Utalii Japhet Hasunga ambapo Waziri Lukuvi   aliwataka wakurugenzi wa a Halmashauri za  Mikoa  hiyo husika kusitisha kupeleka maombi Tamisemi  ya kugawanywa kwa vijiji vipya mpaka migogoro iliyopo itakapo tatuliwa.

Alisema Migogoro mingi iliyopo ni kutokana na vijiji vipya kuanzishwa kiholela na watu wenye maslahi yao binafsi kwa mambo ya siasa na tamaa za madaraka  bila kujua kuwa wanaiingizia serikali hasara ya kutumia fedha nyingi pale wanapoingia kwenye  migogoro.

Waziri Lukuvi alisema Tanzania inayo maeneo makubwa ya Ardhi ila ukubwa huo hautokuwa na manufaa kama matumizi yake hayatozingatia  matumizi bora ya Ardhi ambayo yatakuwa yakiwanufaisha  Wananchi na kutenga maeneo  ya  Wakulima, wafugaji ,  na maeneo ya hifadhi.

 Alisema Wafugaji wengi wanahitaji maeneo makubwa kwaajili ya malisho ya mifugo yao na hiyo ndio sababu ya Wafugaji kuvamia maeneo ya misitu ya Hifadhi, kutokana na hali hiyo imeleta migogoro mikubwa kati wa Wafugaji na wahifadhi misitu, migogoro ambayo inachochewa na uharibifu wa mazingira na upotevu wa uwezo wa Ardhi kuzalisha ,kufungwa kwa shoroba za wanyamapori wanapohama , na kuongezeka kwa ukame.

"Ili kuondoa migogoro hii Wizara na Taasisi imeamua kwa makusudi kuandaa mipango na matumizi bora ya ardhi,  upimaji ambao utawashirikisha wananchi na Wizara zote husika, mipango hii ikifanikiwa wananchi wengi watakuwa na maendeleo makubwa 

 Aidha Waziri Lukuvi alisema sababu nyingine ya migogoro hii ni Wizara husika za Tamisemi, Maliasili na utalii, na Ardhi kutokaa pamoja na kupishana wanapotekeleza majukumu yao ya kugawanya vijiji na kuweka mipaka katika meneo ya hifadhi hivyo baadhi ya vijiji kuanzishwa katika maeneo ya hifadhi na maeneo ya hifadhi kuanzishwa kwenye maeneo halali ya vijiji.

"Migogoro hii huanzia wizarani kwa kutokukaa pamoja na kupanga kwani kwa kutokujua  Serikali ilianzisha makazi katika maeneo ya Hifadhi kwa kugawanya vijiji na  kuna maeneo Serikali imepeleka mpaka  shule na Umeme bila Kujua kuwa eneo lile ni la hifadhi,  sasa tukienda pale kuwafukuza wananchi hawawezi kutuelewa Sasa tunawachanganya wananchi kwasababu Wizara hizi husika hazishirikiani na kufanya kazi pamoja" alisema Lukuvi.

Aliwataka Viongozi wa Mikoa hiyo kutoa ushirikiano ili kufanikisha adhma hiyo ya Hifadhi ya Taifa ya Tanzania na Wizara ya Maliasili kutekeleza mipango wa matumizi bora ya Ardhi kwa kuwafahamisha  na kuwapa elimu juu ya Nia ya na sababu za kuhifadhi maeneo ya wanyama.

Kwa Niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Tanzania Meneja Ujirani kwema hifadhi za Taifa Tanzania Ahmed Mbugi   alisema  sababu ya kufanya  uzinduzi huo ni kutokana na ongezeko kubwa la migogoro siku hadi siku ambao unapelekea kutokuwa na ushirikiano mzuri kati ya Hifadhi na wananchi na Wafugaji na Hifadhi.

 Alisema mpango huo umelengwa kufanywa  tatika hifadhi  16 zilizopo Tanzania  lakini kwa sasa utekelezwaji utaanza katika Mikoa ikiyozunguka Hifadhi tatu za Manyara, Serengeti , Tarangire ambao utahusisha vijiji 95 kati ya vijiji 392 vinavyolengwa.

Naibu waziri Maliasili  na Utalii alisema ili kuwepo kwa matumizi bora ya ardhi ambayo  hayatoleta migongano kati ya wananchi  Hifadhi na Serikali yake lazima viongozi wa Mkoa,Wilaya, viongozi wa vijiji na wataalamu wa ardhi  washirikishwe katika uwekwaji wa Mipaka.

"Tulikuwa tumeagizwa sisi kama Wizara ya maliasili na utalii kwamba hifadhi zetu zote na mapori tengefu tuweke mipaka inayoeleweka kwa kuweka bikon na zoezi hilo wakati linaanza halikuwa zoezi shirikishi ambalo limeleta migogoro katika maeneo mengi" alisema Hasunga. 

" Sasa kama Wizara tumekaa tumeona lazima  tuzingatie sheria na maelekezo, sisi kama Wizara ya Maliasili na utalii ni wahitaji wa Ardhi na wananchi ni wahitaji wa ardhi, hivyo sisi hatuwezi kuonyesha mipaka mwenye mamlaka ya kuonyesha mipaka ni Wizara ya Ardhi wao pekee ndio wanaweza kutuambia kwa Ramani hii Mipaka yetu inaishia wapi" alisema.

Aliongeza kuwa Moja ya njia ya kutatua migogoro  ni kuwa na Mpango shirikishi wa matumizi bora ya ardhi, ili kutofautisha ardhi ya wanyamapori, ya wakulima, na ya Wafugaji na hivyo kuwaachia Wizara ya Ardhi kuonyesha mipaka halali kwani wao pekee ndio wenye Ramani na wanaweza kuonyesha mipaka halali.

(Kwa picha mbalimbali na video angalia sehemu ya  Kituo cha Habari kisha nenda Maktaba ya Picha na Maktaba ya Video)

Imeandikwa na: Haji A.Msovu (Afisa Habari Mkoa wa Manyara)  


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI - BABATI MJI June 29, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI - BABATI MJI June 17, 2022
  • NAFASI ZA KAZI - HALMASHAURI YA MJI WA BABATI May 24, 2022
  • Kanuni za Utoaji na Usimamizi wa Mikopo Kwa Vikundi vya Wanawake, Vijana Na Watu Wenye Ulemavu May 17, 2019
  • Tazama Zote

Habari mpya

  • KIKAO CHA 39 CHA RCC MKOA WA MANYARA

    February 20, 2025
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA MANYARA

    February 19, 2025
  • RC SENDIGA AZINDUA KLINIKI YA MADAKTARI BINGWA MKOANI MANYARA

    November 20, 2024
  • TIMU YA USIMAMIZI WA AFYA MKOA WA MANYARA WAJENGEWA UWEZO KUKABILIANA NA DHARURA ZA KIAFYA NA MAJANGA

    November 14, 2024
  • Tazama Zote

Video

Vuta Pumzi, Funguka, Ongea na Mkuu wa Mkoa
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Miongozo ya OR-TAMISEMI
  • Kanuni za Uchaguzi
  • Mwongozo wa Mfumo wa Anwani za Makazi
  • Mwongozo wa OPRAS
  • Maadili
  • Fomu za Opras
  • Fomu ya Ugonjwa

Tovuti Muhimu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • wizara ya Fedha
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya Wizara ya Elimu
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya Waliotembelea

free HitCounter

Ramani Elekezi

Wasiliana nasi

Mawasiliano mengine

   

    • Sera za Siri
    • Kanusho
    • Ramani Elekezi

Copyright ©2022 Manyara Region Secretariet . All rights reserved.