Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh.Alexander Mnyeti amewataka Wakuu wa mikoa wengine waje kujinza Mkoa wa Manyara katika miradi ya Maendeleo kwani Mkoa huo umeshika nafasi ya pili Kitaifa katika Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 kwa Miradi yote ya Maendeleo kukubaliwa.Mh.Mnyeti ameyasema hayo alipokuwa akimkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan Mkoani Manyara.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh.Alexender Mnyeti amesema shule ya Sekondari Nangwa iliyopo Mkoani Manyara imetengewa Jumla ya Shilingi Milioni Mia nane na Saba kukarabati vyumba kumi vya madarasa,maabara,vyoo,ujenzi wa madarasa mawili, Ukarabati wa Bweni na Ukarabati wa Ofisi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan ameendelea na ziara yake Mkoani Manyara kwa kufungua kiwanda cha Madini aina ya Graphite huko Mirerani Wilayani Simanjiro tarehe 15 Novemba,2018.(Picha Na. Sauda Shimbo)
Haki zote zimehifadhiwa @2017 Mkoa wa Manyara